Latest Posts

MHANDISI MATIVILA ARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI YA BARABARA YA MTILI-IFWAGI

Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu mhandisi Rogatus Mativila ametembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa barabara za Mtili–Ifwagi na Iyegea–Sawala, ambapo ameonesha kuridhishwa na kasi na ubora wa utekelezaji wa miradi hiyo ambayo imefikia asilimia 99.

Barabara hizo, zinazojengwa chini ya Mradi wa wa RISE kupitia mkopo nafuu kutoka benki ya dunia ukiwa na lengo la kurahisisha usafirishaji wa mazao ya chaj, misitu, mbogamboga na mazao mengine kutoka mashambani na kufika sokoni kwa wakati.

Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana, huku akitoa wito kwa wakandarasi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia muda uliopangwa.

Wananchi nao wametoa pongezi kwa serikali kwa kuwaletea maendeleo yanayoonekana na yanayogusa maisha yao ya kila siku.

Barabara hizo zinatarajiwa kurahisisha usafiri, kukuza biashara na kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu kama afya na elimu katika maeneo ya vijijini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!