Latest Posts

MIKAKATI YAWEKWA, UZINGATIAJI MAHITAJI WA WENYE ULEMAVU KATIKA MABADILIKO YA TABIA NCHI DUNIANI

Mfuko wa Dunia wa Watu wenye Wlemavu (Global Disability Fund – GDF) umezikutanisha nchi zaidi ya 23 Mjini Berlin Nchini Ujerumani huku wakijikita katika kuzungumzia masuala yanayohusu Watu Wenye Ulemavu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, Mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi, kukabiliana na kurejesha hali wakati wa maafa pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia

Tanzania imeshiriki mkutano huo huku ikieleza namna Nchi ilivyojipanga kuhakikisha masuala ya Watu Wenye ulemavu yanapewa kipaumbele kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayosaidia katika utekelezaji ya masuala yanayowakabili watu wenye ulemavu

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga ameeleza namna Tanzania inavyozingatia ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali ikiwemo Elimu, masuala ya mabadiliko ya Tabianch, fursa za uongozi, fursa za kiuchumi pamoja na masuala ya kijinsia

Aidha Naibu waziri Nderiananga amesema serikali itaendelea kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu hususani katika athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo uwepo wa maafa yanayoleta madhara mbalimbali ikiwemo vifo, uharibifu wa miundombinu pamoja na athari za kiuchumi

“Sheria ya Usimamizi wa Maafa Sura 242 imeweka uwakilishi wa watu wenye ulemavu kwa Jukwa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa. Vilevile, Kanuni za Usimamizi wa Maafa za mwaka 2022 zinaelekeza kuzingatia mahitaji yao wakati wa kufanya tathmini ya madhara na mahitaji kwa ajili ya kukabiliana na maafa na kurejesha hali,”alisema

Aliongezea kuwa, Sheria ya Usimamizi wa Maafa Sura 242 imeweka uwakilishi wa watu wenye ulemavu kwa Jukwa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa. Vilevile, Kanuni za Usimamizi wa Maafa za mwaka 2022 zinaelekeza kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu wakati wa kufanya tathmini ya madhara na mahitaji kwa ajili ya kukabiliana na maafa na kurejesha hali.

Mkutano huo wa Tatu wa Kimataifa wa Watu wenye Ulemavu Ujerumani, 2025 (Third Global Disability Summit) unafanyika Mjini Berlin, nchini Ujerumani kuanzia tarehe 02 hadi 03 aprili, 2025 ambao umelenga kujadili namna ya kuweka mikakati ya Ujumuishwaji wa masuala ya Watu wenye ulemavu katika nyanja mbalimbali

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!