Latest Posts

MILIONI 369 KUSAIDIA ELIMU NA AFYA SERENGETI NA BUNDA

 

Zaidi ya shilingi Milioni 369 zimetolewa na kampuni ya Grumeti Reserves LTD kwa ajili ya kununua vifaa kwa ajili ya Sekta za Elimu, Afya na Maji kwa jamii zinazozunguka mapori ya akiba ya Ikorongo na Grumeti katika wilaya za Serengeti na Bunda mkoani Mara.

Msaada huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkataba uliosaniwa na shirika hilo na Mamlaka ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania (Tawa) baada ya Grumeti kupewa kitalu kwaajili ya uhifadhi na Maendeleo ya jamii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Grumeti Reserves, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Shirika la Grumeti Fund,Frida Mollel amesema msaada huo ni matunda ya uhifadhi bora hivyo kuhimiza jamii kuhakikisha wanaendeleza uhifadhi na kuepuka vitendo vinavyoweza kuwa chanzo cha uharibifu uhifadhi.

Amesema msaada uliotolewa ni pamoja na madawati 3,014 kwaajili ya shule za msingi, vitanda 21 vikiwemo sita kwaajili ya kujifungulia,kompyuta 21 UPS 8 pamoja na uwekaji wa maji kwa shule moja ya msingi.

“Tumetoa madawati 1,534 kwa wilaya ya Bunda na 1,480 kwaajili ya wilaya ya Serengeti, vitanda 12 kwaajili ya wilaya ya Bunda na vingine vinne kwaajili ya wilaya ya Serengeti pamoja na vifaa vya tehama kwa wilaya zote,” amesema

Amesema kupitia vifaa hivyo jamii inatakiwa kuona umuhimu wa uhifadhi ili kushiriki kikamilifu katika suala hilo huku akisema shirika hilo limepanga kushiriki katika suala zima la maendeleo ya jamii inayozunguka mapori hayo katika kipindi chote cha miaka 20 kwa mujibu wa mkataba waliosaini wakati wa kupewa kitalu hicho.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi kutoka Tawa, Omari Msangi ameziomba mamlaka husika kuhakikisha vifaa vilivyotolewa vinatumika kama inavyotakiwa ili viweze kuleta tija katika jamii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!