Latest Posts

MITI RAFIKI WA MAJI ELFU 50 KUPANDWA BONDE LA USANGU

Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kupitia Mradi wa NBS–USANGU unaofadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Benki ya Dunia, imezindua rasmi zoezi la upandaji wa miti rafiki wa maji 50,000 kwa lengo la kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji katika Bonde la Usangu.

Uzinduzi wa zoezi hilo umefanyika katika Shule ya Msingi Igomelo, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Zoezi hilo linahusisha wanafunzi kutoka shule za msingi 15 zilizopo katika vijiji vinavyonufaika na utekelezaji wa mradi huo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwajengea watoto uelewa wa mapema kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kwa vitendo.

Wanafunzi walioshiriki wameeleza kufurahishwa na kushirikishwa katika zoezi hilo pamoja na elimu waliyopewa na wataalamu wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kuhusu umuhimu wa miti rafiki wa maji katika kulinda vyanzo vya maji.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi endelevu za kulinda rasilimali za maji zinazochangia maendeleo ya sekta za kilimo, uzalishaji wa umeme na utalii katika Bonde la Usangu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!