Latest Posts

MKEMIA MKUU WA SERIKALI KUKUTANA NA WAGANGA WA TIBA ASILI GEITA

Na Theophilida Felician, Geita.

Waganga wa tiba asili na tiba mbadala wanatarajia kukutana na Mkemia Mkuu wa Serikali ili kupewa elimu thabiti juu ya namna ya kuendelea kutoa huduma ya tiba sahihi kwa jamii.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini (TAMESOT), Bw. Lukas Joseph Mlipu, akiwa katika Kata ya Butengorumasa mkoani Geita, wakati akiwahamasisha waganga kuhusu umuhimu wa elimu hiyo kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Amesema mafunzo hayo yanayowalenga waganga wote yana malengo muhimu, ikiwemo kutatua changamoto kadhaa ambazo zimekuwa zikiikabili taaluma ya tiba asili, hususani kutofahamu mbinu salama za uchakataji wa dawa kabla ya kuzipeleka kwa Mkemia Mkuu. Hivyo, ni matumaini yao kuwa kutokana na juhudi mbalimbali za serikali, ikiwemo utoaji wa mafunzo hayo, tiba asili itakuwa bora zaidi kwani itaendeshwa kwa viwango vya utaalamu uliokusudiwa.

Katibu Mkuu huyo amefafanua kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali atatoa elimu hiyo kwa waganga mnamo Machi 23, 2026, mkoani Geita, ambapo ametoa wito akiwasisitiza waganga kutopoteza fursa hiyo adhimu na kushiriki mafunzo hayo ipasavyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!