Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ametoa wito kwa wataalamu na viongozi kuacha kuchukia wanapoona zikisambaa picha za majengo yenye mapungufu na badala yake watafute namna ya kuzitatua changamoto kwa kuwa serikali inaendealea kufanya miradi mingi ya maendeleo.
Mkenda ameeleza hayo mkoani Njombe wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya mji wa Njombe ambapo amesema kumekuwa na ‘clip’ zikionyesha changamoto za miundombinu lakini watumishi hawapaswi kuonyesha chuki badala yake wachukue hatua.
“Hapa na pale kuna Clip zinarushwa madarasa yana matatizo,bado matatizo yapo na hatutafumba macho kwenye haya matatizo na wadhibiti ubora tumewaambia mkiona msilalamike aliyepiga picha leteni na sisi tujitahidi,lakini tusiangalie tu haya mapungufu ambayo hatujayamaliza,angalia tumetoka wapi tumefika wapi ili tujue tunaenda wapi”amesema Prof.Mkenda
Aidha Waziri Mkenda amesema serikali ya awamu ya sita tangu aingie Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan mambo makubwa yameendelea kufanyika hususani kwenye sekta ya elimu ambapo imejengwa miundombinu ya kutosha na kupelekea wanafunzi kuanza masomo kwa mkupuo tofauti na awali walipokuwa wakiingia shuleni kwa awamu.