MJUMBE wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa mkoa wa Rukwa  MNEC Sultan Saleh Seif amempongeza Rais DK Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi  kutekeleza zoezi la mradi wa mipango ya matumizi ya ardhi ngazi ya vijiji wilaya hadi Mkoa ikilenga kupunguza migogoro ya ardhi ya mwingiliano wa matumizi ya ardhi kati ya wawekezaji, wakulima na wafugaji mkoani humo.
MNEC Sultan Saleh Seif ameyasema hayo baada ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Uzingatiaji Matumizi ya ARDHI B Rehema Kishoa kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi Rehema Kishoa kuutambulisha mpango huo kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani humo.
“Mkoa wa Rukwa kumekuwa na migogoro mingi vijijini  kila unapopita utasikia wafugaji hawana maeneo na wakulima wanaingiliwa na wafugaji,mpango huu utatatua changamoto kwa kiasi kikubwa katika mkoa wa Rukwa,
“.alisema MNEC Sultan na kuongeza kuwa.
“Wito wangu Tume ifanye  jambo hili haraka katika kukamilisha mipangilio yao ya mkoa na baada ya kukamilisha wahakikishe wanatoa elimu ya kutosha kwa wanaRukwa kwa ujumla lakini kubwa zaidi ni jambo jema kwa wanaRUKWA kwakuwa mpango utamaliza migogoro ya matumizi ya ardhi kwa watumiajikulingana na makundi husika”.
Aliisitizia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya ARDHI NLUPC kuhakikisha inaendelea kutoa elimu kwa wnanchi ili waweze kuuelewa vizuri mpango huo ambao utakuwa ni suluhisho la migogoro ya ardhi kwa upande wao huku akiishukuru Tume hiyo kuzunguka katika baadhi ya vijijI vilivyonufaika na mpango huo wilayan Sumbawanga katika utekelezaji wa mpango huo.
Akitoa wito kwa wanasiasa Mkoani Rukwa katika suala zima la kuingilia majukumu ya watendaji katika utekelezaji wa mipango ya ardhi ili kumaliza migogoro iliyopo alisema
“Wanasiasa wenzangu jambo hilo la mpango wa matumiziya ardhi ni jambo la kitaalamu kama Wanasiasa tunatakiwa kuwa wepesi sana kuwasikiliza wataalamu wakati mwingine tukiingiza siasa katika masuala ya utatuzi wa migogoro tunaongeza migogoro isiyo ya lazima wito wangu tuhakikishe tunaunga mkoano masuala ya kitaalamu kwa kuzingatia sheria za nchi kwa kutokuleta taharuki inayochangiwa na kutofuata masuala ya kitaalamu,”.
Aliongeza kuwa sheria na miongozi iliyopo inapaswa kuheshimiwa kwa maslahi ya pande zote katika kuwasaidai wananchi na serikali kwa ujumla.