Latest Posts

MPANDA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO KUKAMILIKA KWA SKIMU YA UMWAGILIAJI.

Wakulima katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wanatarajia kuongeza uzalishaji wa mazao kufuatia ujenzi kwa skimu ya umwagiliaji ambayo itawapa uwezo wa kulima hadi msimu mitatu kwa mwaka bila kutegemea mvua.

‎Hayo yamebainishwa na  Samson Rukas meneja wa Mradi wa Umwagiliaji skimu ya Mwamkulu wakati wa ziara ya  Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph, iliyoshirikisha makundi mbalimbali ikiwemo vyama vya siasa kwaajili ya kukagua miradi ya maendeleo  inayotekelezwa na Serikali wilayani humo ili kujionea utekelezaji wake ambayo inaghama ya zaidi ya shilingi 220.

‎Aidha katika kuhakikisha changamoto ya maji inatatuliwa wilaya ya Mpanda wadau hao wametembelea mradi wa miji 28 ambao unatarajia kuongeza uzalishaji wa maji katika mji wa Mpanda na kufikisha uzalishashi wa zaidi ya Lita milioni 15 kwa siku na ililingamishwa na sasa ambapo uzalishaji ni Lita milioni sita.

‎Ziara hiyo imelenga kuwaonesha wadau juhudi na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavyo na wananchi wanapata huduma bora na stahiki.

‎Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza miradi ya kimkakati inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja na amesisitiza umuhimu wa uwazi na ushirikishwaji wa wadau katika miradi ya maendeleo ili kuongeza uwajibikaji na kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali yao.

‎Ziara hiyo imehusisha viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wazee maarufu pamoja na wawakilishi wa makundi maalum wakiwemo bodaboda, bajaji na machinga. Ushiriki wa makundi hayo umeonesha

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!