Jumla ya shilingi bilioni 119 zimetumika katika kutekeleza ujenzi wa mradi wa kimkakati wa wa maji wa chanzo cha mto Kiwila ambapo kukamilika kwake kutaondoa changamoto ya ukosefu wa maji katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake.
Mradi huo ambao ulianza utekelezaji wake mwaka 2023 umefikia asilimia 49 ambapo tayari mkandarasi anaendelea na utekelezaji wa miundombinu ya mradi huo.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurungezi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mbeya Uwsa Mhandisi Barnabas Konga wakati wa ziara ya waandishi wa Habari walipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo katika eneo la Forest mkoani Mbeya ambapo amesema mradi huo utakapokamilika utasaidia kuhifadhi ujazo wa maji wa lita milioni 5 kwa siku jambo ambalo litapunguza kero ya upungufu wa maji katika mji huo.
Kwa upande wake mkandaransi wa mradi huo amba o ni kampuni ya Ukandarasi ya CRCEG -CREC4 Consortion amesema tayari utekelezaji wa mradi huo inaendelea vizuri.
Mradi huo wa maji ulioanza kutekelezwa mwaka 2023 unatarajia kukamilika mwaka 2026.
