Latest Posts

MRATIBU WA THRDC AWAPONGEZA LISSU NA MBOWE KWA KIDEMOKRASIA

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, amekipongeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuendesha uchaguzi wa wazi, huru, na wa kidemokrasia.

Kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa X, Olengurumwa ameeleza kufurahishwa na mchakato wa uchaguzi uliofanyika Januari 22, 2025, akisema kuwa uchaguzi huo ni somo muhimu kwa demokrasia nchini.

“Huu uchaguzi ni elimu tosha ya demokrasia hapa nchini. Nimefarijika sana kuona uchaguzi umeisha kwa haki, uwazi, na uhuru mkubwa. Tumetizama mchakato mzima, hatuna cha kusema zaidi ya kuwapongeza CHADEMA kwa kuendesha uchaguzi kwa misingi ya kidemokrasia,” amesema.

Olengurumwa ametoa pongezi maalum kwa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA taifa, Tundu Lissu, na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akiwapongeza kwa majukumu yao muhimu katika mchakato huo.

“Nakupongeza sana Comrade Mbowe kwa kushiriki uchaguzi na kukubali matokeo, na kuwa tayari kuendelea kujenga chama kama mshauri. Pongezi pia kwa Mhe. Lissu kwa ushindi pamoja na wengine,” ameongeza.

Olengurumwa pia ameeleza kufurahishwa na utulivu wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA wakati wote wa uchaguzi, akisema vyama vingine vina mengi ya kujifunza kutoka kwa CHADEMA. Amehitimisha kwa kuwatakia viongozi wapya kila la heri katika kuimarisha demokrasia nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!