Latest Posts

MSIGWA AONGOZA KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE IRINGA MJINI

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa, Peter Msigwa, ameibuka kuwa wa kwanza kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia chama hicho, katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Iringa Mjini, Msigwa amesema  amesukumwa kuwania nafasi hiyo kwa dhamira ya kupaza sauti ya wale ambao kwa muda mrefu wamekuwa hawana nafasi wala uwakilishi wa karibu.

“Nimeamua kusimama kwa ajili ya wananchi wa Iringa Mjini, hasa wale wa chini ambao hawana sauti. Nataka kuwawakilisha na kuwatetea ndani ya Bunge,” alisema Msigwa .

Wengine waliojitokeza kuchukua fomu ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Iringa, Fadhili Ngajilo, ambaye alisema azma yake ni kuendeleza mji wa Iringa kwa kushirikiana na wananchi katika maendeleo endelevu pamoja na kada wa chama hicho Nguvu Chengula

“Ninajua changamoto zinazowakabili wananchi wa Iringa Mjini. Naamini nina uwezo wa kusaidia kuzitatua kupitia nafasi ya ubunge,

Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Hassan Makoba, aliwataka wote wanaochukua fomu kufuata utaratibu wa chama, ikiwemo kutoanza kampeni kabla ya muda rasmi.

“Tunawahimiza wagombea wote kuzingatia maadili ya chama. Hatutavumilia yeyote atakayeanza kampeni kabla ya wakati au kuendesha kampeni za matusi na kejeli,” alionya Makoba.

Zoezi la uchukuaji wa fomu linaendelea huku kukitarajiwa ongezeko la wagombea wengine kujitokeza .

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!