Latest Posts

MTENDAJI ALIYEWAFUKUZA WAANDISHI WA HABARI MISENYI ATAKIWA KUOMBA RADHI NDANI YA SIKU SABA

Theophilida Felician, Kagera.

Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kagera (KPC) imeeleza kusikitishwa na kitendo cha mtendaji wa kata ya Kanyigo, wilaya ya Misenyi Daud Kyaka ambaye alishuhudiwa akiwadhalilisha waandishi wa habari Theophilida Felician wa Redio Karagwe na Pontian Kaiza wa Kasibante Fm mbele ya kikao cha cha wadau wa maji Julai 11, 2024 wakati wakitimiza majukumu yao ya kitaaluma.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti (KPC) Mbeki Mbeki, waandishi hao walienda kwa mwaliko maalumu kwa ajili ya kutimiza wajibu lakini mtendaji akawafukuza.

Mwenyekiti (KPC) Mbeki Mbeki

“Bila kujali taaluma yake na wajibu wake kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa kata, alichukua hatua ya kuwafukuza kwenye kikao kwa vitisho na maneno makali ya kuwadhalilisha waandishi hao” Ameeleza Mbeki.

Mtendaji Kyaka alichukua hatua hiyo akidai kuagizwa hilo na Mkuu wa Wilaya wa Missenyi Kanali mstaafu Hamissi Mayamba Maiga ambaye alikanusha kutoa maagizo hayo.

Kutokana na suala hilo, uongozi wa KPC umesema utamwandikia barua mtendaji huyo na kumtaka kuiomba radhi KPC ndani ya siku (7) kuanzia tarehe 17 Julai, 2024, na endapo atakaidi KPC imeeleza kuwa haitasita kutoa msimamo wao kama waandishi na wanachama wa Kagera Press Club (KPC).

“Kagera Press klabu imesajiliwa chini ya wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania, Jukumu lake kubwa ni kuhakikisha maadili ya kihabari yanazingatiwa, amani na usalaama kwa wanahabari unakuwepo na wanafanya kazi zao kwa uhuru bila kuingiliwa huku wakifuata maadili ya kazi na taaluma yao” Ameeleza Mbeki.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!