Latest Posts

MTENGA AWATAKA VIONGOZI CCM KUACHA MATABAKA

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mtwara wametakiwa kuacha kufanya kazi kwa matabaka, kuchukiana na badala yake washikamane ili waweze kushinda kwa kishindo kwenye chaguzi zijazo.

Hayo yameelezwa na mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini Hassan Mtenga alipokuwa anazungumza na wanachama wa kata mbalimbali zilizopo manispaa ya Mtwara Mikindani kwa nyakati tofauti.

Mtenga amesema, kumekuwa na matabaka kwa baadhi ya viongozi wa chama hiko na kusababisha kutokuwa na umoja ndani ya chama hali inayoweza kusababisha kushindwa katika chaguzi zijazo kutokana na changamoto hiyo.

“Siku zote ukiona jimbo limeanguka wanaoangusha ni wana-CCM, kata ikianguka ujue wana-CCM na hata mtaa pia na hii yote ni kutokana na matabaka yaliyopo kwenye chama tukishirikiana  wenyewe kwa wenyewe hatutopata kazi kwenye chaguzi zetu kuanzia serikali za mitaa, madiwani, mbunge hadi kwa Rais.”

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mtwara mjini Salumu Naida, amewataka wanachama kuwaheshimu viongozi waliopo madarakani kwa kupewa dhamana na wananchi pia waache kuwatia moyo wale wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali kuwa watachaguliwa.

Aidha amewataka wanachama hao kuendelea kuwaunga mkono viongozi waliopo madarakani ambao wanafanya kazi kwa uadilifu na kuleta maendeleo ili waendelee kuwepo na kuwaongoza.

Nae mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Mtwara mjini Karimu Chilumba, amewataka wanachama kufanya kazi ili kuweza kujipatia kipato na kuacha ujanja ujanja wa kuwaaminisha watu kuwa utampa cheo.

“Hakuna tabia mbaya ndani ya chama kama tayari yupo kiongozi lakini wewe unamuaminisha mtu kuwa nitakupa cheo fulani labda nitakupa udiwani au nitakupambania uwe mbunge ili mradi tu uchukie senti zake, jamani tufanye kazi, kazi ziko nyingi” Amesema Chilumba.

Sambamba na hilo Mtenga ameendelea kutoa vifaa vya ujenzi wa ofisi za serikali za mitaa na ofisi za CCM ambapo kata ya Reli ametoa tofali 500 saruji mifuko 10 mabati 30 na kata ya Magomeni ametoa tofali 1000 na mifuko 30 ya saruji.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!