Latest Posts

MTOTO AZAMA SHIMO LA MAJI TAKA, MWINGINE AZAMA BAHARINI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linachunguza matukio mawili ya vifo vya watoto wawili waliofariki dunia kwa kuzama katika mazingira tofauti.

Katika tukio la kwanza, mtoto Victoria Mlongwesi (1 1/2), mkazi wa Kijiji cha Mbuo, Kata ya Ndumbwe, Wilaya ya Mtwara, alifariki dunia baada ya kuteleza na kutumbukia kwenye shimo la maji taka (karo) lililokuwa wazi wakati akicheza na watoto wenzake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Issa Suleiman, tukio hilo lilitokea Machi 17, 2025, majira ya mchana.

Katika tukio jingine, mtoto Mudasiru Hassan (10), mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mgao, Kata ya Naumbu, Wilaya ya Mtwara, alifariki dunia baada ya kuzama katika Bahari ya Hindi akiwa anaogelea na wenzake.

Tukio hilo pia lilitokea Machi 17, 2025, wakati wa mapumziko ya shule, ambapo marehemu alikwenda kuogelea baharini pamoja na wanafunzi wenzake katika eneo jirani na shule hiyo.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa matukio hayo huku likitoa wito kwa wazazi na walezi kuwa waangalifu zaidi katika kulinda usalama wa watoto wao. Aidha, limewataka wananchi kuhakikisha mazingira wanayoishi yanakuwa salama kwa watoto ili kuepusha matukio yanayohatarisha maisha yao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!