Latest Posts

MUSTAKABALI WA DHAMANA YA BONIFACE JACOB WA CHADEMA KUJULIKANA LEO

Mustakabali wa dhamana ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo Boniface Jacob (Boni Yai) unatarajiwa kujulikana leo, Jumanne Oktoba 01.2024, saa 03 asubuhi, Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam
Boni Yai ambaye pia ni kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) awali dhamana yake ilitarajiwa kutolewa Septemba 23.2024 na Septemba 26.2024 lakini mara zote hizo mbili (2) ilikwama kutokana na uwepo wa sababu tofauti ikiwemo sababu za kiusalama na zile za kisheria
Shauri hilo leo litaletwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusomwa kwa hukumu ya maamuzi madogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili mshtakiwa huyo
Hoja zinazotarajiwa kutolewa maamuzi na Mahakama ni pamoja na kwamba kama kiapo cha RCO wa mkoa wa Kipolisi Kinondoni kilichowasilishwa Mahakamani hapo kimewasilishwa ndani ya muda stahiki na kama kimewasilishwa kwa mujibu wa sheria au la, na kwamba endapo kiapo hicho kimewasilishwa ndani ya muda stahiki na kwa kufuata msingi ya kisheria je, Boniface Jacob anastahili kupewa dhamana au la
Ikumbukwe kuwa, msingi wa kuwasilishwa kiapo hicho unatokana na hoja za Jamhuri/ serikali zilizowasilishwa Mahakamani hapo zinazodai kuwa usalama wa Boniface Jacob (Boni Yai) uko shakani endapo atasalia ‘uraiani’ hivyo Mahakama hiyo inaombwa kutompatia dhamana licha ya kwamba makosa yanayomkabili yanadhamika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!