Latest Posts

MVUA KUBWA KIGOMA: UNICEF YATOA MSAADA KWA KAYA 411 ZILIOATHIRIWA, RC KIGOMA AUKABIDHI KWA MANUSURA

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye, amekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mkoani Kigoma kati ya Desemba 2023 hadi Aprili 2024.

Mafuriko hayo yaliathiri Halmashauri za Uvinza, Kigoma, na Manispaa ya Kigoma Ujiji, na kusababisha kaya 411 kuhama makazi yao.

Baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Wakuu wa Wilaya hizo, Andengenye amewasisitiza viongozi kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na inatumika kama ilivyokusudiwa. Pia, amewataka wananchi wa Kigoma kuepuka kujenga katika maeneo ya mabondeni ili kujikinga na madhara ya mvua yanayoweza kuhatarisha maisha na mali zao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Ofisi ya UNICEF Mkoa wa Kigoma, Justus Ndenzako, ametaja vifaa vilivyotolewa kuwa ni magodoro 200, ndoo 300, mablangeti 310, vyandarua 100, na mashuka 10, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 20.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Dinnah Mathamani, ameishukuru UNICEF kwa msaada huo na kuahidi kuhakikisha vifaa hivyo vinawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa. Aidha, ameomba wadau wengine kuungana na serikali ya mkoa katika kutoa misaada kwa manusura wa mvua hizo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!