Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi amefanya ziara katika wilaya ya Iringa vijijini na kupita katika matawi kwa lengo la kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kuhamasisha usajili katika matawi hayo.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Mlenge na Itunundu jimbo la Ismani mkoani Iringa Mwamwindi amesema, ziara hiyo ya kamati ya utekelezaji ya UWT Mkoa wa Iringa inapita Wilaya zote nne kuhakikisha wanawake wa mkoa mzima wanahamasika na kugombea katika chaguzi hizi za serikali za mitaa .
“Niwapongeze sana UWT wilaya ya Iringa vijijini kwa kuendelea kufanya ziara mbalimbali katika kata zenu na sisi UWT Mkoa wa Iringa tupo kwenye ziara hii ambayo italeta chachu kubwa ya wanawake kushiriki katika kugombea uchaguzi huu wa serikali za mitaa.”