Latest Posts

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA NISHATI SAFI SOKO LA SAMAKI FERRY

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ussi, leo ameongoza uzinduzi wa mradi wa Nishati Safi ya kupikia katika Soko la Samaki Ferry, Jijini Dar es Salaam, na kuhimiza jamii kuachana na matumizi ya nishati chafu kama mkaa na kuni kwa ajili ya kulinda afya na mazingira.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyohudhuriwa na wananchi, wajasiriamali na viongozi wa Serikali, Ismail Ussi amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kila Mtanzania anapata nishati safi, rafiki kwa mazingira na salama kiafya.

“Tumeona juhudi kubwa zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Samia katika kuhakikisha Watanzania wanapata nishati safi ya kupikia. Kupitia mikakati na sera madhubuti, Serikali imerahisisha upatikanaji wa gesi majumbani na kuwekeza kwenye teknolojia rafiki kwa mazingira. Hii ni ishara ya uongozi wenye maono na kujali maisha ya wananchi,” amesema Ussi.

 

Mradi wa Gharama ya Milioni 216

Mradi huo umetekelezwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Kampuni ya Oryx Gas kwa gharama ya Shilingi milioni 216. Lengo kuu ni kupunguza utegemezi wa nishati chafu, kupunguza gharama za uendeshaji kwa wajasiriamali, kulinda afya ya watumiaji pamoja na kuhifadhi mazingira ya Bahari ya Hindi na maeneo ya karibu.

Kwa mujibu wa viongozi wa soko hilo, mradi umepokelewa kwa mikono miwili na wafanyabiashara ambao wamesema utasaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya mfumo wa hewa, kuharakisha shughuli za usindikaji wa samaki, na kuongeza ufanisi wa biashara.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!