Latest Posts

MWENYEKITI WA BODI YA USHAURI DKT. LEONARD AKWILAPO AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KAMPASI YA MBEYA

 

Iwambi, Mbeya
05 Septemba, 2024

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Dkt. Leonard Akwilapo na Mtendaji Mkuu Dkt. Maulid J. Maulid leo tarehe 5 Septemba, 2024 wamefanya ziara maalumu kutembelea na kukagua ujenzi wa jengo la kuendeshea mafunzo katika Kampasi ya Mbeya.

Jengo hilo la ghorofa moja lenye kumbi nne za mihadhara zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 500 kwa mara moja na ofisi za watumishi limegharimu kiasi cha Shilingi 1,500,000,000.00 mpaka sasa na litagharimu kiasi cha shilingi 1,700,000,000.00 mpaka litakapokamilika.

Dkt. Akwilapo amemtaka fundi mjenzi SUMA JKT kuhakikisha anakamilisha sehemu zilizobaki katika ujenzi huo na kukabidhi mradi huo kwa Menejimenti ya Wakala haraka iwezekanavyo kwani mradi huo ulitakiwa kuwa umekamilika katika mwaka wa fedha 2023/2024 na kumtaka Mtendaji Mkuu Dkt. Maulid J. Maulid na Menejimenti ya kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ili ifikapo septemba 21, 2024 Fundi Mkuu akabidhi jengo hilo likiwa limekamilika.

Ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi mwaka 2021 chini ya fundi Mkuu SUMA JKT na fundi Mshauri TBA ambao watakabidhi mradi huo kwa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi ADEM ukiwa umekamilika mnamo tarehe 21 Septemba, 2024.

ADEM Kampasi ya Mbeya inatarajiwa kuhamia rasmi katika jengo hilo lililopo katika eneo la Iwambi Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika muhula wa masomo 2024/2025.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!