Mkuu wa mkoa wa Tabora Paulo Chacha ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Itilo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nzega Mji wilayani Nzega mkoani Tabora kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Paschal Kigalu  yamefanyika leo February 19,2026 Wilayani humo.
Paschal kigalu alifariki dunia usiku wa kuamkia Februari 17,2026 kufuatia ajali ya barabarani ambayo imehusisha gari alilokua amepanda kugongana na gari jingine wakati alipokuwa kwenye mizunguko yake binafsi.
Akizungumza na waombolezaji Rc Chacha mbali na kutoa pole amewataka kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki kigumu pamoja na kuwasisitiza kuyaenzi yale mazuri aliyokua akiyafanya marehemu katika jamii , Kata na halmashauri kwa ujumla kwa mustakabali wa maendeleo ya eneo hilo.
