Latest Posts

NAIBU WAZIRI MAHUNDI AWASAIDIA WAFUNGWA GEREZA LA RUANDA

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya na Mkurugenzi wa Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF), ametekeleza ahadi yake ya kusaidia wafungwa na mahabusu wa Gereza la Ruanda, lililopo jijini Mbeya.

Septemba 27, 2024, Mahundi ametoa vifaa vya michezo, ikiwamo mipira na seti mbili za sare, pamoja na tanki la maji lenye ujazo wa lita elfu tano kwa ajili ya kusaidia gereza hilo.

Aidha, Mahundi ameahidi kuendelea kuwasaidia wafungwa hao kwa kuwanunulia magodoro pamoja na kusaidia ujenzi wa bweni maalumu kwa ajili ya wafungwa wanawake.

 

Mkuu wa Gereza la Ruanda, Kamishna Msaidizi Sinjonjo Mwakyusa, ameishukuru Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation pamoja na ofisi ya Mbunge Mahundi kwa msaada huo, akisema kuwa utasaidia kuboresha afya za wafungwa na mahabusu gerezani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!