Latest Posts

NAIBU WAZIRI WA FEDHA ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula, ametembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano pamoja na taasisi zake, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, jijini Tanga.

‎Akiwa katika banda hilo, Mhe. Luswetula alipatiwa maelezo kuhusu majukumu na shughuli zinazotekelezwa na Idara na Vitengo mbalimbali vya Ofisi hiyo, ikiwemo masuala ya kinga ya jamii, usajili wa vyama vya waajiri na wafanyakazi, kukuza tija na ubunifu kazini pamoja na utoaji wa huduma za ajira.

‎Aidha, amewapongeza watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano pamoja na taasisi zake kwa juhudi zao za kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusu huduma wanazozitoa, hususan katika kipindi cha maadhimisho hayo.

‎Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo amehimiza wananchi kutumia fursa ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano ili kujifunza na kupata uelewa mpana wa shughuli zinazotekelezwa na ofisi hiyo.

‎Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanafanyika chini ya kauli mbiu isemayo: “Elimu ya Fedha Msingi wa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!