Latest Posts

KAHAMBA: MSITUMIE BIMA YA AFYA KWA MTU ZAIDI YA MMOJA

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Mtwara, Adolf Kahamba amewataka watumiaji wa bima kutotumia kadi za bima kwa mtu zaidi ya mmoja kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria .

Ameyaeleza hayo kwenye hafla fupi ya ugawaji wa kadi za bima ya afya kwa wanawake wajane 100 waishio mkoa wa mtwara zilizotolewa na Taasisi isiyokuwa ya serikali mkoani Mtwara ya Nanauka Foundation ambapo meneja huyo amesema kadi hizo zipo tayari kufanya kazi kuanzia hivi sasa na ni za kipindi cha mwaka mmoja.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Joel Nanauka amesema bima hizo zimegharimu shilingi milioni 30 na wameguswa kufanya hivyo kutoka na changamoto nyingi wanazokutana nazo wanawake hao kwani wengi wao hukosa msaada kwenye familia zao.

Amesema wamewakatia bima hizo kwa ajili ya kuwasaidia kupata matibabu ndani na nje ya mkoa wa Mtwara kwasababu ni bima kubwa hivyo wanaweza kwenda hadi hospitali za rufaa, ghafla iliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo.

“Mtwara tuna wajane 100 lakini pi tuna mikoa mingine na kwa takwimu zinaonyesha tanzania mzima tuna wajane karibu laki nane na elfu themanini ambao karibia asilimia 3.1 ya wananchi wote wa Tanzania.”Amesema Nanauka

Aidha kwa Mkoa mzima wa mtwara pekee kuna wajane 5,000 na kikubwa kinachofanywa taasisi hiyo ni kuona wanawafikia wadau wengine kuja kuwasaidia wajane hao.

Hata hivyo wajane  hao wengi wao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo magonjwa sugu kama vile kansa, kisukari na mengine yanayohitaji msaada mkubwa ikizingatiwa wengi wao hawana kipatao cha kijitosheleza.

Meneja wa NHIF mkoani Mtwara, Adolf Kahamba amewasisitiza wajane hao kutotumia kadi hiyo kwa mtu zaidi ya mmoja na zipo tayari kufanya kazi kuanzia hivi sasa na ni za kipindi cha mwaka mmoja.

Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Sixmund John amesema ni faraja kubwa kwa wanamtwara kuona wadau kama hao wanafanya mambo mengi ya kijamii ikiwemo hilo lililofanyika la kuona na kutambua mahitaji ya watu wenye mahitaji wakiwamo wajane hao.

Mratibu wa Wajane Kanda ya Kusini, Sesilia Erio amewaomba wajane hao kuendelea kutambua mchango mkubwa unaofanywa na taasisi hiyo kwa mtu au watu pamoja na vikundi mbalimbali ikiwemo wajasiliamali na kutoa shukrani kutokana na vile taasisi hiyo inavyojali makundi hayo.

Baadhi ya wajane hao akiwemo Felister Joseph mkazi wa kata ya majengo kwenye manispaa hiyo, “Tunafurahi sana wajane kwa msaada huu mkubwa wa kutusaidia matibabu kwasababu wakati mwingine  tunaumwa lakiki hatuna ela matibabu”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!