Latest Posts

NDUGU WASHINDWA KUMSAIDIA BI. ZULEKHA KISA TAMADUNI KUTORUHUSU

Zulekha Ahmed Ibrahim (60), mkazi wa mtaa wa Salum Abdallah maarufu kama Juwata, wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro amejikuta akiishi kwa kutengwa na ndugu anaoishi nao katika kaya moja licha ya kuwa mzee na mgonjwa wa miguu hali iliyopelekea wakati fulani kujisaidia haja zake mahali anapolala ambako ni mabanda ya uani mithili ya stoo.

Zulekha ambaye ni mhindi kikabila na mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya marehemu Ibrahim, alikua ameolewa na mumewe ambaye ni marehemu kwa miaka mingi sasa, alipata matatizo ya miguu na ndipo alipoamua kutoka kwake na kuishi nyumba ya familia na dada zake akitarajia msaada kwa ndugu zake lakini hali ikawa tofauti.

Amekuwa akiishi kwa kuwekwa kwenye mabanda ya uani peke yake bila kusaidiwa chochote wala kupatiwa mahitaji ya msingi ya binadamu ikiwamo chakula na usafi binafsi pamoja na mazingira, ndugu zake wakikataa kumsaidia kwa sababu wanasema kufanya hivyo ni kinyume cha tamaduni zao.

Baada ya kugundua hilo Mkaguzi Kata ya Kingo A/Insp willneema Sule alikwenda kwenye nyumba hiyo na kuzungumza na dada (ndugu) hao akitaka kumuona Zulekha lakini walimkataza mpaka pale alipowaeleza umuhimu wa yeye kama polisi jamii kufahamu mambo hayo na wakamuelewa.

Ilikuwa ngumu kwa Sule kumsaidia hivyo alilazimika kuutafuta uongozi wa kata akiwamo Afisa jamii wa Kata na kuwasiliana na ndugu wengine wa Zulekha ambao walikuja na kutoa huduma za kuogeshwa na kupewa chakula, na baadaye ndugu hao walimpeleka hospitali huku wakikubali kumchukua ili awe kwenye mazingira rafiki zaidi.

A/Insp Willneema Sule ameahidi kuendelea kupita mara kwa mara eneo hilo kujua afya yake lakini pia kumsaidia awe anapata fedha za kujikimu kupitia kodi/pango kutoka kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu mume wake ambazo zilidaiwa kuchukuliwa na ndugu yake mwingine, ambapo polisi wamesema watahakikisha Zulekha anapata stahiki zake zote na kurudi katika afya bora.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!