Latest Posts

NGASHA AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA NG’APA AKIAHIDI BIDII KATIKA UTUMISHI WAKE

Mgombea mteule wa nafasi ya udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Ng’apa, Jimbo la Lindi Mjini, Ndugu Issa Ngasha, amewaomba wananchi wa kata hiyo kuiamini CCM na kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Ng’apa katika uzinduzi rasmi wa kampeni uliofanyika Septemba 29, 2025, Ngasha amesema atatumia nafasi hiyo kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi wa kata hiyo zinatatuliwa.

Ngasha pia amewaomba wananchi waendelee kumuunga mkono Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya urais, Mohammed Utaly kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini, pamoja na yeye mwenyewe kwa nafasi ya udiwani.

“Mimi ni kijana wenu mliyenilea. Tukishirikiana, nitapeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi kwa uaminifu na sitowaangusha ndugu zangu wa Ng’apa,” alisema.

Uzinduzi huo uliambatana na shamrashamra na hamasa kubwa kutoka kwa wanachama wa CCM na wakazi wa kata hiyo ambapo mgeni rasmi, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Lindi Mjini, Ndugu Jamadin Mandoa, amewasihi wananchi kumuunga mkono Ngasha, akimwelezea kama kiongozi mwenye maono, uaminifu na uzoefu wa kutosha.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!