Latest Posts

WANAWAKE SENGEREMA WAFUNGUKA KUHUSU HAKI NA USAWA

Wanawake Wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameeleza kuwa kufikia haki na usawa wa kijinsia bado ni safari ndefu, wakisema uhalisia wa mfumo wa kijamii unaendelea kumpa nafasi kubwa mwanaume katika maamuzi ya familia na jamii.

Wakizungumza na Jambo TV katika mahojiano maalumu kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, baadhi ya wanawake hao wamesema licha ya kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana ni Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050,” bado wanakumbana na changamoto mbalimbali zinazowarudisha nyuma.

“Tunasema haki na usawa lakini ukweli haipo baba atabaki kuwa baba na ndio maana anapendelewa sehemu nyingi unakuta baba lazima apewe kipaumbele katika shughuli za kijamii hata tukiwa kwenye mkusanyiko wa kijamii unakuta lazima wababa wapewe kipaumbele,” amesema Happness Shija Mkazi wa Mtaa wa Jeshini.

Akizungumza kuelekea maadhimisho hayo ambapo kwa wilaya hiyo yamefanyika jana, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga amesema mbali na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha usawa na haki lakini bado baadhi ya wanawake hujidharau na kutokujikubali.

“Changamoto tuliyonayo kubwa huwa tunajidharau na kujiona hatuwezi tunaishia kusema wanawake tunaweza lakini ukweli ni kwamba ni kweli tunaweza na tusijidharau sisi ni wa thamani kubwa na tunaweza kufanya mambo makubwa,” amesema Ngaga

Kwa upande wake, Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu amesisitiza umuhimu wa maadili katika jamii, akiwataka wazazi kuwalea watoto katika misingi ya dini na maadili mema.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Sengerema, Peragia Joseph ametaja baadhi ya changamoto wanazokumbana wanawake wilayani humo ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!