Latest Posts

NGUO, NYAVU ZILIZOISHA MUDA WAKE JANGA JIPYA ZIWA VICTORIA

Wakati juhudi za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira katika vyanzo vya maji zikiendelea kuelekezwa zaidi kwenye taka za plastiki, wataalamu wa mazingira wameibua tishio jipya la uchafuzi wa Ziwa Victoria linalotokana na nguo na nyavu zilizokwisha muda wake wa matumizi kutupwa ziwani.

Akizungumza na Jambo TV wakati wa zoezi la kusafisha na kuondoa taka katika mwalo (ufukwe) wa Igombe uliopo Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Blue Victoria, Festus Massaho, amesema tatizo hilo linaongezeka katika maeneo mengi ya mwambao wa ziwa huku likiwa halipewi uzito mkubwa kama ilivyo kwa taka za plastiki.

 

“Tumeshazoea au tumeshasikia mara nyingi wakitaja plastiki kwenye maziwa au kwenye vyanzo vya maji lakini nawaambia kuna kitu kingine ambacho hakizungumzwi ambacho nguo pamoja na nyavu ambazo zimeisha muda wake wa matumizi kutupwa ziwani,”

Massaho amesema tangu zoezi la kusafisha na kuondoa taka kwenye mialo na fukwe lianze mkoani Mwanza wamefanikiwa kuondoa karibia tani za Nyavu zilizokuwa zimetelekezwa kwenye visiwa viwili.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mwalo wa Igombe wilayani Ilemela, Thadeo Philipo, amesema uwepo wa shughuli mbalimbali za kibinadamu kandokando ya ziwa zilizopigwa marufuku na Serikali husababisha uchafuzi na uharibifu wa mazalia ya samaki ziwani.

Hata hivyo nao baadhi ya wavuvi katika mwalo huo wa Igombe wamesema kutokana na uchafuzi kukithiri ziwani hata upatikanaji wa samaki umepungua.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!