Latest Posts

NINAWAOMBA CHADEMA WAICHAGUE CCM KAMA WANAPENDA MAENDELEO- NJEZA.

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Oran Njeza (CCM), amesema kuchagua viongozi wanaogombea nafasi mbalimbali kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiyo kuchagua maendeleo badala ya vyama vya upinzani.

Njeza amesema hayo wakati akiwanadi wagombea wa nafasi za uenyekiti na ujumbe wa Serikali za Mitaa, vitongoji na vijiji katika kijiji cha Njelenje, kata ya Mshewe, Mbeya Vijijini.

Mbunge Njeza amewataka wananchi kuhakikisha kwenye uchaguzi huo wanawachagua wagombea wa CCM akisema awamu hii CCM imesimamisha wagombea imara hivyo watasukuma gurudumu la maendeleo.

“Ndugu zangu kuna mtu anataka porojo hapa, bila shaka wote tunahitaji maendeleo, na kama tunataka maendeleo ni lazima tuje wapi CCM. CCM safari hii nawashukuru sana viongozi wangu wa Chama wamesimamisha wagombea wazuri kweli na haya majembe haya (wagombea) mimi nitayatumia na nyie mnitumie kwasababu kila kitu kitakuja huku kwasababu mimi kwa niaba yenu mwenyekiti wetu wa chama Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuheshimisha Mbeya vijijini mimi ndiye mwenyekiti wa kamati ya bajeti na fedha wa bunge la nchi hii. Asikudanganye mtu hata hao CHADEMA na mgombea wao hapa Njelenje namuomba kama anapenda maendeleo aichague CCM ila kama hapendi maendeleo abaki hukohuko CHADEMA”, ameeleza Mbunge huyo wa Mbeya vijijini na mwenyekiti wa wabunge mkoa wa Mbeya.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!