Latest Posts

NIPO TAYARI KUZUNGUMZA YA OKTOBA 29 WATAYAWEZA? – LISSU, MAHAKAMANI

Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam inatarajiwa kutoa uamuzi wa kama ni sahihi au lah kupokelewa kwa notisi ya ushahidi wa ziada kwenye ushahidi wa shahidi wa 26 katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu, ACP Amini Mahamba.

Shauri hilo linalosikilizwa na jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru leo Februai 23, 2026 mara baada ya shauri kuanza upande wa Jamhuri kupitia Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga uliieleza mahakama kuwa unataka kuwasilisha notisi ya ushahidi wa ziada ya shahidi ambae ni Askari Mpelelezi ACP Amini Mahamba ambae alikuwa Mpelelezi kiongozi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

Wakili Katuga alisoma maelezo ya notisi hiyo akieleza kuwa mnamo Februari 18, 2026 kwa njia ya mtandao wali-file notisi ya kuongeza ushahidi kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 mapitio ya 2023 ambapo pia waliiambatanisha na kiini cha ushahidi huo.

Katuga aliieleza Mahakama kuwa notisi hiyo ni ushahidi wa nyongeza wa shahidi anaeitwa ACP Amini Mahamba na ushahidi huo haukuwekwa na kusomwa wakati shauri likisomwa mwenendo kabidhi(commital proceedings).

Katuga ya alieleza Mahakama kuwa ACP Amini Mahamba ndie aliyekuwa kiongozi wa timu ya upelelezi wa matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu na baada ya na kile alichokipata kutokana na upelelezi ndicho kilichopo kwenye kiini cha nyongeza ya ushahidi wake.

Lissu aliieleza Mahakama kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ni kuwa ni shahidi ambae hakuwa kwenye maelezo ya ushahidi wakati yanasomwa kwenye mahakama ya ukabidhi ndiyo yanayopokelewa na si kuongezwa kwa ushahidi wa shahidi ambae alishatoa ushahidi wake.

Lissu aliendelea kuieleza mahakama kuwa si sahihi kupokea ushahidi huo pia kwani unazungumzia matukio yaliyotokea Oktoba 29 na baada yake haliyakuwa yeye makosa aliyoshtakiwa nayo yalitokea April 3, 2025, akakamatwa April 9 na kushtakiwa April 10 na kuanzia hapo amekuwa akishikiliwa gerezani.

“Ni ushahidi wa mtu aliefanya upelelezi wa Matukio ya Wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 na siku zilizofuata mimi tayari nilikuwa mahabusu kwa takribani miezi sita 6 na nusu mimi nimekuwa nguvuni tangu April 9, 2026 Jamhuri inataka kuleta mambo ambayo hayapo kwenye hati ya mashtaka kwa kuwa Jamhuri inataka kuleta ushahidi wa matukio ya uchaguzi mkuu wakitaka kuthibitisha malalamiko ya April 3, 2026”

Aidha Lissu alieeleza mahakama kuwa pamoja na kwamba hakubaliani na notisi hiyo lakini pia yupo tayari kuzungumzia yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi.

“Nipo tayari kujadili ya Oktoba 29 watayaweza?  Oktoba kulikuwa kuna mauaji ya halaiki na ni magumu” alisema Lissu huku akiiomba mahakama kuikataa notisi hiyo.

Upande wa Jamhuri kupitia Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga ulizijibu hoja za Lissu wakiendelea kusisitiza juu ya uhalali wa kuwasilisha notisi hiyo na kwamba haubadili hati ya mashtaka kama ambavyo Lissu amedai.

Baada ya ubishani wa hoja za pande zote Mahakama imesema kesho saa tatu asubuhi itatoa uamuzi na wa juu ya kupokelewa kwa notisi hiyo na kisha ushahidi utaendelea.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!