Latest Posts

PANYA MABALOZI WALIOTOKA SUA: KUTOKA MOROGORO HADI MAREKANI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameeleza mafanikio makubwa ya mradi wa mafunzo ya panya wanaotambua mabomu na vimelea vya kifua kikuu, maarufu kama “panyabuku”, unaoendeshwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia mradi wa APOPO.

Akisoma makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 bungeni jijini Dodoma siku ya Jumatatu, Prof. Mkenda amesema hadi sasa panya 100 wamefundishwa, kufuzu mafunzo, na kupelekwa katika nchi mbalimbali kwa kazi maalum za uokozi na afya.

Prof. Mkenda amesema kati ya panya 100 waliopata mafunzo hayo, 13 wamepelekwa Angola, 11 nchini Azerbaijan, 58 nchini Cambodia, 6 nchini Ethiopia

Panya hao hutumika kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini katika nchi zilizoathiriwa na migogoro ya kivita pamoja na kugundua vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu.

Aidha, amesema panya 12 wamepelekwa Marekani kama mabalozi wa maonesho ya wanyama katika mashamba ya wanyama (zoos), wakiiwakilisha Tanzania kimataifa.

Katika mafanikio hayo, Prof. Mkenda ameeleza kwa fahari kuwa panya wa Kitanzania aitwaye Ronin amevunja rekodi ya dunia kwa kutambua mabomu 109 yaliyotegwa ardhini nchini Cambodia. Rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na panya mwingine wa Kitanzania Magawa aliyewahi kutambua mabomu 71.

Amesema utekelezaji wa mradi huo umeendelea kuijengea sifa Tanzania na kuitangaza kimataifa kwa kuwa miongoni mwa nchi chache zinazofundisha wanyama kwa ajili ya kusaidia katika sekta ya usalama na afya.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!