Theophilida Felician, Kagera.
Vyombo za usalama mkoa Kagera viameahidi kutoa ushirikiano wakutosha kwa shirika linalojishughulisha na masuala ya utunzaji wa amani nchini INTERNATIONAL PEACE INFORMATION (IPI) katika masuala mbalimbali ikiwemo ya utoaji taarifa za uchunguzi kiusalama.
Vyombo hivyo vimetoa kauli hiyo mbele ya Rais wa shirika hilo Taifa Mh Prof Wilson George Munguza alipofika ofisi za mamlaka hizo kwa ajili ya kuwatambulisha viongozi wa shirika mkoa Kagera na wilaya zake.
Utambulisho huo umefanyika ofisi za mamlaka ya usalama mkoa ambazo ni jeshi la Polisi, Uhamijai, Zima moto na uokoaji sambamba na Takukuru ambapo kila chombo kimepokea vyema ujio wa shirika hilo kutokana na malengo yake yakujikita kuisaidia serikali katika suala zima la utunzaji wa amani na mengineyo ya husuyo uchunguzi wa taarifa za usalama kwa kushirikiana na vyombo hivyo.

Hatahivyo wakuu wa Idara hizo wameahidi kuwa ofisi zao zitajitolea masuala kadhaa ikiwemo suala la kutoa mafunzo ya elimu kwa wana IPI ili kuwaongezea ujuzi zaidi kwa lengo la kuwaweka sawa na kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Aidha Rais wa shirika Prof Munguza amevipongeza na kuvishukuru vyombo hivyo kwa mapokezi mazuri ofisi zote ambapo amewahakikishia kazi ya kuisaidia serikali masuala ya uchunguzi na kuitunza amani yatafanyika kikamilifu maeneo mbalimbali ya nchi kama ilivyokusudiwa na shirika hilo linalofanya kazi na nchi za Afrika mashariki na makao makuu yake yakiwa ni mkoani Dare es salaam.