Latest Posts

POLISI: WINFRIDA HAJATEKWA, AMEKAMATWA KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji limesema mwanamke anayesambazwa mitandaoni akidaiwa kutekwa na watu wanaodaiwa kujitambulisha kama askari wa Kibiti, Winfrida Charles Malembeka, hajakumbwa na tukio la utekaji, bali amekamatwa kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uchochezi na kuhamasisha vurugu kupitia mitandao ya kijamii.

Katika taarifa iliyotolewa Novemba 28, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Protas Mutayoba, imeelezwa kuwa Winfrida alikamatwa katika maeneo ya Kibiti Mjini na kwa sasa anaendelea kushikiliwa na jeshi hilo mpaka taratibu za kisheria zikamilishwe.

“Anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uchochezi, kuhamasisha vurugu na maandamano tarehe 09/12/2025 kupitia mitandao ya kijamii akishirikiana na watu wengine”, imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kuepuka kuchapisha na kusambaza taarifa za kichochezi zinazoleta taharuki kwa jamii, likisisitiza kuwa halitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!