Theophilida Felician Kagera.
Vijana mkoani Kagera na Tanzania kwa ujumla wametakiwa kuwa makini nakuwaepuka watu wanaoweza kuwashawishi ili kushiriki matendo ya vurugu zenye kuihatarisha amani ya nchi hususani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba.
Wito huo umetolewa na viongozi wa taasisi ya mabalozi wa amani Tanzania PPAÂ yenye makao yake manispaa ya Bukoba.
Viongozi hao wakizungumza na vyombo vya habari wamefafanua kwamba nyakati kama hizi kundi la vijana huonwa kama kundi muhimu hivyo hujikuta wakitumiwa na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa kwa malengo yakuwavusha katika harakati zao za kisiasa na wengine huwatumia ndivyosivyo hali inayopelekea kuwepo kwa matukio yavurugu hadi uvunjifu wa amani.
Maulid Rashidi Kambuga ni mkurugenzi wa taasisi amesema amani ikishatoweka hakuna pakukimbilia iwe kwa vijana, wazee, akina mama, watoto wote wanaathirika.
Naye Mchungaji Clavery Venant ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa PPA amebainisha kuwa kundi la vijana hawanabudi kuishi kwa hofu ya Mungu na kuzingatia misingi ya maadili mema.
Bahati Ildephonce ni mkazi wa Bukoba yeye ameeleza kuwa amani ikishavunjika husababisha madhara mengi kwa jamii hasa maumivu, vifo, kuteteleka kwa uchumi na miundo mbinu.
Kwa pamoja wametoa wito kwa wananchi kuwa wazalendo wa kweli ili kuilinda nakujenga Tanzania ya amani kwani Tanzania ni moja tuu ikishaponyoka hakuna kimbilio.