Meneja wa Mfuko wa Hifadhi Ya Jamii Kwa Watumishi Wa Umma (PSSF) Kanda ya kusini Lulyalya Sayi amewasisitiza waajiri ambao bado wanamadeni ya nyuma waweze kulipa ili na wao waweze kutimiza wajibu wa kulipa mafao.
Sayi ametoa msisitizo huo wakati wa Mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na mfuko huo wa pssf yaliyolenga kutoa elimu kwa waandishi hao kuhusu mfuko huo ulipoanzia hadi sasa ulipofikia.
Amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili ni waajiri kutowasilisha michango kwa wakati hali inayopelekea ucheleweshaji kwa wanachama na baadhi ya waajiri kuwa na malimbikizo ya madeni na kusababisha wao kutotimiza wajibu wao wa kulipa mafao kwa wanachama.
Ameongeza kuwa lengo la kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ni kufikisha ujumbe kwa walengwa ambao ni wafanyakazi na jamii kwa ujumla ukizingatia waandishi ni wadau wakubwa ambao wakielewa watafikikisha na kutoa elimu ipasavyo.
Akieleza mafanikio waliyopata toka kuanzishwa kwa mfuko huo mwaka 2018 hadi sasa ni kumrahisishia mwanachama kulipwa mafao yake kwa muda mfupi zaidi kwa kutumia huduma za kidijitali ambapo pia mwananchama mpya anaweza kujiunga kupitia huduma hiyo ya kidijitali.
Smythiea Pangisa ni miongoni mwa wanufaika wa mfuko wa pssf kutoka mkoa wa Mtwara ameupongeza uongoza wa pssf kwa kukamilisha malipo ya wastaafu kwa wakati bila changamoto.
Kwa upande wake Mussa Mtepa amesema kitendo cha pssf kupata huduma zao kwa mfumo wa kidijitali itarahisishia wanachama wake na kuongeza idadi ya wanachama pia amewapongeza kwa kushughulikia changamoto ya ucheleweshaji wa mafao kwa wanachama wao ambapo kwasasa ndani ya siku 14.