Latest Posts

RAILA ODINGA AFARIKI DUNIA

Kiongozi wa upinzani na Waziri Mkuu wa zamani nchini Kenya Raila Odinga amefariki dunia leo Oktoba 15, 2025 akiwa na umri wa miaka 80, hii ni kwa mujibu wa taarifa za Vyombo mbali mbali vya habari vya Kenya na India

Imeelezwa Raila amefariki wakati anapokea matibabu katika Hospitali ya Ayurvedic eneo la Koothattukulam, Kerala, nchini India.

Kabla ya taarifa za kifo chake kuthibitishwa, kulikuwa na uvumi mtandaoni kwamba kiongozi huyo amefariki, lakini familia yake ilikanusha na kusema alikuwa akipata nafuu.

Raila atakumbukwa kwa msimamo wake imara kuhusu demokrasia, haki za binadamu na mageuzi ya kitaifa, na alibeba matumaini ya Mamilioni ya Wakenya waliotamani mabadiliko ya kisiasa.

Kiongozi huyo wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), alikuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mwaka 2007 hadi 2013. Pia amewahi kuhudumu kama Waziri wa Nishati chini ya Rais Daniel arap Moi (2001-2002) na kama Waziri wa Barabara, Ujenzi na Makaazi chini ya Rais Mwai Kibaki (2003-2005)

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!