Latest Posts

RAIS SAMIA ANATARAJIWA KUWA MWENYEKITI WA JUKWAA LA VIONGOZI WAKUU NCHI ZA AFRIKA NA CHINA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Viongozi wakuu wa nchi za Afrika na China mkutano unaotarajiwa kuanza tarehe 4-6 Septemba 2024.

Katika ziara hiyo nchini China Rais pia atashiriki mkutano wa wakuu wa Nchi na Serikali wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambapa atahutubia ufunguzi wa mkutano huo.

Akiwa nchini China Rais Samia atafanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Xi Jinping na kushuhudia uwekaji saini wa hati za makubaliano ya uboreshaji wa Reli ya TAZARA na baadaye kukutana na kampuni na wawekezaji kutoka China ili kuhamasisha uwekezaji zaidi nchini Tanzania.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!