Latest Posts

RAIS SAMIA KULETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA MFUMO WA KODI NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa kiongozi wa kwanza tangu Rais Benjamin Mkapa kuboresha mfumo wa kodi nchini Tanzania, kutokana na kuunda Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi.

Tume hiyo inalenga kushughulikia changamoto za mfumo wa kodi na kutoa mapendekezo ya kuboresha ukusanyaji na matumizi ya kodi.

Moja ya malengo muhimu ni kuimarisha uwazi na uwajibikaji wa usimamizi wa kodi ili kujenga imani ya wananchi kwa serikali na mfumo wa kodi, ambao mara nyingi umekuwa ukikabiliwa na malalamiko kuhusu ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Tume pia itazingatia mbinu mpya, ikiwemo teknolojia ya kisasa, kwa lengo la kuongeza mapato ya serikali bila kuathiri wananchi. Mfano wa teknolojia hiyo ni mifumo ya kielektroniki inayorahisisha malipo ya kodi na kuondoa urasimu usio wa lazima.

Akizungumza siku ya Ijumaa Oktoba 04, 2024 Ikulu, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Tume hiyo, Rais Samia amesisitiza ushirikiano na sekta binafsi katika kuboresha mfumo wa kodi na kuimarisha mazingira ya biashara yanayovutia wawekezaji.

Imeelezwa kuwa mazingira ya biashara yanavutia wawekezaji na kuimarisha uchumi wa nchi, jambo ambalo ni muhimu katika kipindi ambacho uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto, na Tanzania ikihitaji kuongeza mapato yake ya ndani ili kufikia malengo yake ya maendeleo

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!