Latest Posts

RAIS WA MALAWI ATANGAZA KIFO CHA MAKAMU WAKE KATIKA AJALI YA NDEGE

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ametangaza kuwa mabaki ya ndege iliyokuwa imembeba aliyekuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo Seulos Chilima na maafisa wengine wa serikali ya nchi hiyo yamepatikana lakini taarifa za kusikitisha ni kwamba hakuna mtu yeyote aliyenusurika kwenye ajali hiyo.

Saulos Chilima na maafisa wengine tisa walikuwa wakisafiri nchini humo Jumatatu Juni 10, 2024 asubuhi wakati ndege waliyokuwa wanasafiria ilipotoweka kwenye rada za uwanja wa ndege, ambapo taarifa za awali zilieza kuwa ndege hiyo kijeshi ilikuwa ikisafiri kwenye mazingira ya hali mbaya ya hewa.

Maafisa wa Jeshi la Malawi wanatajwa kufanya kazi ya ziada ya kupekua msitu wa Chikangawa katika juhudi za kuitafuta ndege hiyo.

Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa shirika la habari la kimataifa la Uingereza (BBC) Jumanne Juni 11, 2024 imenukuu taarifa ya Rais Chakwera aliyoitoa kwenye kikao chake na wanahabari ambapo ameleza kuwa Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Malawi alimueleza kuwa shughuli ya utafutaji na uokoaji imekamilika na mabaki ya ndege hiyo kupatikana. Rais Chakwera amesema timu ya uokoaji imekuta ndege hiyo ikiwa imeharibika kabisa

Ikumbukwe kuwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima na Rais wa nchi hiyo Lazarus Chakwera ni wanasiasa wanaotoka kwwnye vyama viwili (2) tofauti vya siasa lakini wawili hao waliungana kuunda muungano wakati wa uchaguzi wa mwaka 2020.

Hayati Chilima (51) na msafara wake wamefikwa na ajali hiyo iliyokatisha maisha yao wakati wakielekea kuiwakilisha serikali katika mazishi ya aliyekuwa Waziri wa serikali Ralph Kasambara aliyefariki siku chache  zilizopita.

Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye ndege hiyo iliyoruka kutoka mji mkuu wa Malawi Lilongwe ni pamoja na mke wa Rais wa zamani wa Malawi Shanil Dzimbiri. Awali ndege hiyo ilikusudiwa kutua kwenye uwanja wa ndege katika mji wa kaskazini wa Mzuzu lakini inaelezwa kuwa ilirudishwa kwa sababu ya hali mbaya ya hewa

Hayati Chilima amekuwa Makamu wa Rais wa Malawi tangu mwaka 2014, ambapo enzi za uhai amekuwa miongoni mwa wanasiasa waliopendwa sana nchini humo, hasa miongoni mwa vijana

Aidha, Hayati Chilima alikamatwa na kufunguliwa mashtaka mwaka 2022 kwa madai ya kwamba alikubali pesa ili kutoa kandarasi za serikali. Mwezi mmoja uliopita Mahakama ilitupilia mbali mashtaka hayo, bila kutoa sababu za uamuzi huo

Hadi umauti unamkuta Chilima ameacha mke na watoto wawili (2).

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!