Latest Posts

RAS NJOMBE: TOENI USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WA S/MITAA NA VIJIJI

News, Njombe.

Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Judica Omari, amewataka wananchi mkoani humo kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali za mitaa na vijiji ambao wameanza kazi baada ya kukamilika kwa zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa lililofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Judica ametoa wito huo wakati wa sherehe za maadhimisho wa miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika kimkoa katika viwanja vya posta mjini Njombe kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kupanda ya matunda na vivuli, kufanya mazoezi pamoja na usafi kwenye kituo cha afya Njombe Mjini.

Judica pia ametumia fursa hiyo kuishukuru kamati za ulinzi wa usalama za mkoa na wilaya kwa kuhakikisha zoezi hilo linafanyika katika hali ya usalama bila vurugu.

“Viongozi wetu wote wamechaguliwa kwa haki na ushiriki wa wananchi ulikuwa ni mkubwa sana na kwa asilimia kubwa, lakini viongozi katika ngazi zetu zote za vijiji, mitaa, vitongoji zoezi lilienda vizuri,” amesema Judica.

Aidha Katibu Tawala, amesema kuwa uongozi mpya umeanza kufanya kazi kwa kutekeleza majukumu ya kuendeleza maendeleo na wananchi wanachohitaji hivi sasa ni maendeleo na kuishi kwa usalama ili kazi zao za uchumi ziweze kwenda vizuri.

“Ninachoomba tutoe ushirikiano wa hali ya juu, tushikamane pamoja na hawa viongozi waliochaguliwa katika mamlaka zetu za serikali za mitaa ili kuhakikisha kwamba serikali yetu inaongozwa salama lakini maendeleo zaidi yanaenda kupatikana,” amesema Judica Omary

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!