Latest Posts

RC CHALAMILA AELEZA NAMNA ‘DADA POA’ WATAKAVYOSAIDIWA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameonesha kuchukizwa na wanaolalamikia kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuwakamata ‘dada poa’ na ‘kaka poa’ akirejea mijadala ya watoto waliohudhuria maadhimisho ya Mtoto wa Afrika kwamba ni muhimu kwa watoto kupata malezi bora kutoka kwa wazazi wao hivyo kitendo kilichofanyika kilikuwa njia ya kuwalinda watoto.

RC Chalamila ameonesha hali hiyo alipokuwa akizungumza katika viwanja vya Karimjee Alhamisi Juni 20, 2024 ambapo amesema ni fedheha kubwa sana kwa Tanzania na hata baadhi ya nchi za Afrika kutafsiri maisha ya kawaida ya baba au mama ‘kujiuza’ muda wao mwingi wa maisha na kusahau malezi ya watoto kisha hivyo kuna haja ya kutafuta njia za kuleta suluhu kwenye suala hilo mtambuka.

“Tunachokifanya ni kubadilisha fikra na tulichokifanya kwenye halmashauri zetu ni kuanza kuandaa mikopo maalumu itakayowasaidia wale wenye mawazo ya kuuza miili yao na kufanya vitendo ambavyo bado haviakisi utamaduni wetu, ili waweze pia kujimudu na kufanya biashara zingine ambazo zitakuwa na mwangwi mzuri wa watoto wetu kuiga kutoka kwa wazazi wao” Amesema Chalamila.

Aidha Chalamila ameonya kile alichokiita kushabikia ujinga kwa watu wachache ambao wanahisi wanawake waliokamatwa kwenye msako wa Mkuu wa Wilaya kuwa walidhalilishwa huku akirudia kusisitiza nukta yake kwamba walichukuliwa na kuhudumiwa katika namna walivyokutwa pasina kufanyiwa kitu cha tofauti.

“Ukweli ni kwamba hakuna mama hata mmoja aliyevuliwa nguo, nguo walijivua wenyewe hakuna mama hata mmoja aliyefanyiwa vitendo hivyo bali walichukuliwa kama walivyovaa wenyewe, wakiwa wamekaa hadharani kwa watu wenyewe, na wakiwa wamewaacha watoto nyumbani wenyewe na kupelekwa mahali ambapo patasitirika ili pasiwe aibu kwa watoto wanaopita asubuhi alfajiri kwenda shuleni na baadhi ya maeneo mengine” Ameeleza Chalamila.

Katika hatua nyingine RC Chalamila amesikitishwa na vitendo vya ukatili vinavyoendelea nchini na kuamua kutangaza kuanzisha operesheni maalumu ya kamata waganga wa kienyeji jijini Dar es Salaam baada ya tukio la mtoto mwenye ualbino wilayani Muleba mkoani Kagera kuuawa na kisha viungo vyake kupelekwa kwa mganga wa kienyeji kwa sababu ya imani potofu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!