Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amezindua Kamati ya Uwekezaji mkoa wa Dar es Salaam katika ofisi za Kituo cha Uwekezaji (TIC), Kanda.
RC Chalamila ameiagiza Kamati hiyo kutekeleza malengo yake kwa ufanisi na kuzingatia masuala mbalimbali ya uzalishaji, masoko, usafirishaji, kuhakikisha uwekezaji endelevu ili kufanikisha uwekezaji sanjari na biashara kwenye mkoa wa Dar es Salaam.
Kamati hiyo ya Uwekezaji ya mkoa inaundwa na Taasisi mbalimbali 15 na Wajumbe 19, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Dkt. Toba Nguvila ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, na Katibu wa Kamati ni Fidelis Obanga kutoka TIC.