Latest Posts

RC MARA AWATAKA CHADEMA KUKEMEA MAUAJI KWENYE JAMII

Mkuu wa Mkoa wa Mara Col Evans Mtambi amekutana na katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Tarime Vijijini Zablon Mrimi nakumtaka katibu huyo kutumia mikutano wanayoifanya kukemea Mauaji ya mtu na mtu ambayo yamekuwa yakifanyika Wilayani humo nakuchafua Mkoa wa Mara.

Mtambi amemtaka Katibu huyo wa CHADEMA kutumia majukwaa yake kuielimisha jamii ya Tarime kuendelea kukemea vitendo ambavyo vimekuwa vikijitokeza ikiwemo wananchi kuchomana vitu vyenye ncha kali huku zikisababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo wivu wa mapenzi na migogoro mbalimbali ya kijamii.

Pia Col Mtambi amesema haipo Serikali ambayo itakubali uhai wa mwananchi wake kuondokewa na mtu ama watu kwa sababu zinazozuilika ambapo amesema anahakikisha Mkoa wa Mara unaondokana na picha hiyo kwa kutoa elimu kutokana na wananchi wake kuwa wapenda Maendeleo.

“Elimisheni jamii watu wabadilike kuna njia nyingi ambazo ni suluhu kukabiliana na haya Matukio na ulinzi ni wa kila mtu simaneni nanyie mkemee hatutaki kuona haya yakitokea kwenye Mkoa wetu.

Kwa upande wake katibu wa Chadema Jimbo la Tarime Vijijini Zablon Mrimi amekubali kupokea ushauri wa Mkuu wa Mkoa nakuahidi kutoa ushirikiano kwani jamii ya Wilaya ya Tarime ni jamii ambayo inafanya kazi kubwa ambapo amesema atakuwa sehemu ya kuhamasisha kuondoka na vitendo hivyo na watu wake kujikita na uzalisha kupitia kilimo kutokana wilaya hiyo kusaidia kwa kiasi kikubwa katika chakula katika mikoa jirani.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mara Col Mtambi ameagiza kuundwa Mabaraza ya ushauri kila Wilaya ambayo hayahusiana na yale ya ardhi yatakayosaidia kukabiliana na vitendo hivyo huku yakitakiwa kutokutoa adhabu yoyote.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!