Katika kuendelea na juhudi za kutunza mazingira mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameagiza kila kaya Mkoa wa Katavi kupanda miti ya kupendezesha mazingira pamoja na ya matunda ambayo pia itasaidia katika kampeni kupambana na changamoto ya udumavu katika Mkoa wa Katavi.
‎katika tukio hilo taarifa iliyosomwa kuhusu zoezi la upandaji miti imebainisha kuwa mpaka sasa Manispaa imepanda miti zaidi ya laki sita ikiwepo miti ya matunda katika mmakazo ya watu na ofisi na taasisi mbalimbali na zoezi hilo ni endelevu.
‎
‎Ameagiza kila mwananchi na taasisi zilizokabidhiwa miti kuhakikisha wanazipanda na kuzihudumia Ili kuendelea kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira ambazo zimekuwa na matokeo chanya kwa Mkoa wa Katavi ikiwemo mradi wa hewa ya ukaa.
‎Mkoa wa Katavi kwa mwaka 2026 unatarajia kupanda jumla ya miti milioni kumi ikiwemo miti ya kivuli miti ya kupendezesha mazingira pamoja na miti ya matunda ambapo mpaka sasa zadii ya miti milioni tatu tayari imepandwa ambapo mkuu wa Mkoa amesisitiza utunzaji wa miti hiyo
