Latest Posts

RDO MAFINGA YATOA MAFUNZO KWA WALIMU NA WADAU WA UMEME

Shirika la Maendeleo la Rural Development Organization (RDO) limeandaa mafunzo maalum kwa walimu na wadau wanaojishughulisha na shughuli za umeme nchini. Mafunzo haya, yanayodumu kwa siku mbili, yanalenga kuimarisha ujuzi wa wadau hao wanaofundisha katika vyuo mbalimbali vilivyosajiliwa na NACTIVET.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, mkufunzi Michael alisema kwamba mafunzo haya ni fursa ya kukumbushana jinsi umeme unavyofanya kazi na pia kuongeza maarifa mapya katika eneo hilo.

Michael alifafanua kwamba RDO imekuwa ikitekeleza mafunzo haya mara kwa mara ili kuwawezesha walimu kupanua ujuzi wao na kuboresha utoaji wa elimu kwa walimu na wadau wa umeme.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa RDO, Fidelisi Filipatali, alisema kuwa shirika lake lina taratibu za kuandaa mafunzo mbalimbali, ambapo lengo kuu ni kutoa fursa kwa walimu na wadau wa umeme kupanua maarifa yao.

Filipatali aliongeza kuwa mafunzo haya, yanayoendeshwa na mkufunzi Michael kutoka nje ya nchi, yatawasaidia walimu wa vyuo vya RDO kuongeza ujuzi wao na pia kujikumbusha mambo muhimu kuhusu umeme.

“Tunayo taratibu zetu za utoaji mafunzo kwa walimu na wadau wa umeme. Tunafanya hivi ili kukumbusha mambo yanayohusu umeme na kuboresha ujuzi wao,” alisema Filipatali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!