Latest Posts

RUWASA NAMTUMBO WAGAWA PIKIPIKI MBILI NA DIRA ZA MAJI 20 KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Namtumbo yagawa pikipiki Mbili (2) na Dira za maji ishirini (20) ili kuwezesha Usimamizi wa Huduma ya maji vijijini

Wenyeviti wa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii kutoka kata ya Lusewa jumuiya ya MSILU na SAMALIA kutoka kata ya Magazini wamepatiwa pikipiki Mbili kutoka kwa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, kwa ajili ya kusimamia miradi ya maji.

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Haruna Mang’uli amekabidhi pikipiki hizo katika kata ya lusewa na Magazini uku akisisitiza kutunza na kuzitumia vizuri ili ziwezeshe kutatua changamoto mbalimbali za upatikani wa Huduma ya Maji.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Namtumbo, Mhandisi David Mkondya akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya watumiaji Maji ngazi ya jamii (CBWSOs) katika kata za Lusewa na Magazini amesema lengo la kutoa vitendea kazi hivyo ni kwa ajili ya kutumika na kusimamia miradi ya maji

“Lengo la Rais Samia Suluhu Hassan kumtua ndoo kichwani na limefanikiwa kwa kiasi kikubwa pia kupitia vitendea kazi hivi tutafanya kazi ya kusimamia miradi ya maji ipasavyo,” amesema Mkondya.

Said Zidadu Diwani wa kata ya Lusewa ameishukuru Serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) kutoka Wilaya ya Namtumbo kwa kutoa chombo cha usafiri (pikipiki) kwani uwepo wa chombo hicho cha Usafiri kitawezesha ufanikishaji wa majukumu ya ufuatiliaji ikiwemo kutatua changamoto mbalimbali za Dosali katika upatikanaji wa Huduma ya Maji.

Hata hivyo Zidadu ameiomba Serikali kupitia RUWASA kuongezewa miondombinu ya Maji ikiwemo Matenki ili kuwezesha kuondoa kabisa changamoto ya maji katika kata ya Lusewa, uku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kuifadhi, kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji ikiwa na pamoja ka kuepuka ukataji miti katika maeneo mbalimbali

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!