Latest Posts

SAUTI YA WATANZANIA WATAKA KUACHIWA KWA SOKA NA WENZAKE

Vuguvugu la Sauti ya Watanzania limemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutumia mamlaka yake ya kikatiba na kisheria kutoa maagizo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi ili vijana wanaosemwa kutoweka kusikojulikana wapatikane na kuachiwa mara moja.

Kupitia kile walichokichapisha kama barua ya wazi kwa Rais Samia tarehe 21 Agosti 2024 kwa sahihi ya mwakilishi wa Sauti ya Watanzania Albin Saragu, vijana waliopotea ni Deusdedith Soka, Jacob Godwin Mlay, na Frank Mbise ambao wanaelezwa kutekwa nyara mnamo Agosti 18, 2024 katika eneo la Buza, Dar es Salaam.

Ripoti za awali zinaonesha kwamba vijana hao walidanganywa kupitia simu, wakielekezwa kufika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe kuhusu pikipiki iliyopotea mwaka jana, tukio ambalo limefananishwa lile la utekaji na jaribio la mauaji ya Edgar Mwakabela (Sativa).

“Tangu kutekwa kwa vijana hawa watatu, hakuna taarifa yoyote kuhusu walipo au hali zao, jambo ambalo limeleta mshtuko mkubwa kwa familia zao, marafiki, na jamii nzima ya Watanzania”, imeeleza barua hiyo.

Aidha barua hiyo kwa Rais Samia, imedai uchunguzi wa kina kubaini “maafisa waliohusika katika utekaji” huo na kuchukua hatua madhubuti za kuzuia matukio kama hayo yasitokee tena, na ikidai utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Jaji Chande iliyopendekeza mabadiliko makubwa katika Jeshi la Polisi.

“Matukio ya utekaji nyara yameongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni, na ikiwa hukubaliani na kuunga mkono vitendo hivi, tunaamini kwamba utachukua hatua za haraka kusimamia haki, kuhakikisha usalama wa raia wote wa Tanzania, na kurejesha imani katika utawala wa sheria. Hatua za haraka zinahitajika ili kuleta matumaini na amani kwa familia za vijana hawa na jamii kwa ujumla”, imeeleza barua hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!