Latest Posts

SERIKALI KUANDAA UTARATIBU WA KUTAMBUA MCHANGO WA VIJANA WANAOJITOLEA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu amesema Serikali inaandaa utaratibu rasmi wa kutambua mchango wa vijana wanaojitolea kwenye taasisi mbalimbali za serikali huku akiwataka vijana hao kuwa wavumilivu na wasikatishwe tamaa.

Sangu ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza katika mkutano ya hadhara uliofanyika katika Kata ya Ikozi na Kalambanzite zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipouteliwa kushika wadhifa huo.

Amesema utaratibu huo utasaidia kupata watu sahihi wanaojitolea badala ya kupata mamluki ambao hupenyezwa na ndugu zao pindi fursa za ajira zinapojitokeza.

Amesema udanganyifu huo umekuwa ukifanywa na  baadhi ya watumishi wasio waaminifu wenye ndugu zao na kupelekea  manung’uniko kwa vijana sahihi wanaojitolea

Kufuatia hatua hiyo, Sangu amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ipo katika hatua ya  mwisho wa kuandaa utaratibu huo ambao utakuwa mwarobaini wa namna bora wa kutambua mchango wa vijana hao.

Katika hatua nyingine, Sangu amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na hivyo kupelekea  baadhi ya watumishi ambao sio waaminifu kuanza kufuja fedha hizo.

Kufuatia hatua hiyo Sangu ameielekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwabana watumishi hao ili kukomesha tabia hiyo.

Hata hivyo Sangu amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaendelea kuwasimamia watumishi wote nchini ili kuhakikisha fedha za miradi ya maendeleo zinapopelekwa kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo  zinasimamiwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa

“TAKUKURU hakikisheni mnawabana watumishi ambao ni wadokozi wa  fedha  za miradi ya maendeleo inayotolewa na Rais wetu”, amesisitiza Sangu

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!