Latest Posts

SERIKALI YACHIMBA VISIMA VIREFU KUSAIDIA WANANCHI WA BUGWEMA, MUSOMA KUPATA MAJI SAFI

Serikali imepeleka mtambo wa uchimbaji visima virefu katika vijiji vya Jitulola na Masinono vilivyopo kata ya Bugwema, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara. Mradi huu unalenga kuchimba visima viwili virefu, ambavyo vitawanufaisha takriban wakazi 15,000, na kutatua changamoto ya ukosefu wa maji safi katika eneo hilo.

Wananchi wa vijiji hivyo, wakizungumza kwa nyakati tofauti, wameishukuru serikali kwa jitihada zake, kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya maji. Mara nyingi walilazimika kugawana maji na mifugo, jambo lililokuwa gumu kwao.

“Tunaishukuru sana serikali kwa kutuletea mradi huu wa visima virefu. Umefika wakati muafaka na utatupunguzia adha kubwa tuliyokuwa tukipitia,” alisema Mwamvua Josephat, mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Musoma, Mhandisi Edward Sironga, alisema kuwa mtambo huo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha upatikanaji wa maji safi katika maeneo yenye changamoto. Jumla ya visima virefu vitano vinatarajiwa kuchimbwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kupitia mradi huu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!