Baada ya shahidi wa saba P2 (38) katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kumaliza kutoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Ignas Mwinuka, Lissu alimsomea shahidi maelezo aliyoandika polisi kisha kumueleza maeneo ambayo ana wasiwasi nayo na kumtaka kuwasilisha kwa majaji kama kielelezo ambapo yalipewa jina E6.
Lissu alianza kumhoji shahidi juu ya maeneo kadhaa ikiwemo juu ya atatambulikaje kama mfuasi wa CHADEMA haliyakua hana utambulisho wowote.
Lissu alimtaka shahidi kuwaelezea majaji kama wafuasi huwa wana alama usoni iliyoandikwa chadema akajibu sijui. Alipoulizwa kama ana kadi ya CHADEMA pia akajibu hana.
Akamuuliza kama huna kadi ya chadema na huna alama Jaji atajuaje kama we ni mfuasi wa CHADEMA?. Shahidi akajibu kwa kusema sijui kwa ufahamu wao.
Baada ya hapa Lissu alimuuliza shahidi kama amewahi kutishwa na wafuasi, viongozi au wanachama wa CHADEMA, ambapo awali alikataa lakini baadae alisema vitisho vipo mtandaoni. Lissu alitaka kufahamu ni nani wanaomtisha P2 akasema kuwa hawafahamu.
Simulizi nzima ya shahidi huyu utaikuta YouTube ya JAMBO TV.