Latest Posts

SHAURI LA UCHOCHEZI LA LISSU LAAHIRISHWA KWA MUDA USIOJULIKANA

Shauri na. 8606/2025 la uchochezi linalomhusu Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Tundu Lissu limeahirishwa kwa muda usiojulikana mpaka pale mashauri mawili ya mapitio yaliyofunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania yatakapotolewa uamuzi.

Tundu Lissu alifungua mashauri mawili- moja likiwa la kurejewa kwa uamuzi wa Mahakama ya Kisutu kutokutoa uamuzi juu maombi ya Lissu kupinga mashahidi kutoa ushahidi wa kificho na kudai kuwa unahatarisha haki yake ya kusikilizwa kwa haki na ukamilifu.

Shauri la pili lililofunguliwa Lissu linapinga mambo ambayo yaliiruhusu serikali kuleta mashahidi wake kwa kificho kuwa hapakuwepo na ushahidi wa kutosha kumuwezesha Hakimu kutolea uamuzi wa kuruhusu kutolewa kwa ushahidi wa kificho kwa watu ambao sio askari

Mashauri hayo mawili yalisikilizwa na Jaji Elizabeth Mkwizu Juni 28, 2025 na yanatajiwa kutolewa maamuzi Julai 11, 2025.

Upande wa Utetezi uliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upo tayari kuendelea na shauri hilo bila kusubiri uamuzi wa Mahakama Kuu kwa sababu mashauri ya Mahakama Kuu hayahusiani na mashahidi ambao sio askari hivyo waliitaka mahakama kuendelea na mashahidi ambao ni askari.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!